Fursa ya Kipekee ya Kusaidia Maendeleo ya Nishati Safi ya Kupikia ya Umeme Nchini Tanzania – Kwa Nafasi ya Kampuni Mshirika

MECS

Tanzania 05/07/24 -29/07/24

Descriptions



Kampuni ya MECS inafuraha kutangaza zabuni kwa nafasi ya
Kampuni Mshirika ili kusaidia utekelezaji wa mradi wa kuendeleza matumizi ya
Nishati Safi ya Kupikia ya Umeme. Mradi huo unaofadhiliwa na FCDO, na kuungwa
mkono na Wizara ya Nishati Tanzania, fursa hii ya zabuni iko wazi kupitia
tovuti ya manunuzi ya Delta eSourcing. Waombaji wote watahitajika kujisajili
kama wasambazaji na kutumia msimbo A6M279HE2X1 kupata maelezo. Zabuni hii iko
wazi kwa kampuni mshauri yoyote yenye sifa, au shirika, kutoka Tanzania.
Mshindi wa zabuni (mmoja au timu) atahitajika:



  Awe anaendesha
shughuli zake ndani ya nchi wakati wa mradi huo.



Aweze
kufanya kazi kwa kushirikiana na wengine ili kuhakikisha kunakuwa na utendaji
wa hali ya juu na kwa wakati.



•Asaidie
kutoa elimu kuhusu mradi huo na kukuza ushiriki wa wadau, kuhakikisha ushiriki
katika ngazi za juu kwenye Wizara za Serikali na taasisi nyingine za kitaifa.



Pendekezo linapaswa kuanisha siku zisizozidi 15 kwa mwezi,
kwa muda usiozidi miezi 17 na liwe na thamani isiyozidi £95,000. Mkataba
unatarajiwa kuanza Septemba 2024 na kuendelea hadi Januari 2026. Kwa maelezo
zaidi, Semina mtandao ya MECS itafanyika Alhamisi 11 Julai saa 7:30 mchana kwa
saa za Afrika Mashariki (maelezo zaidi tembelea www.mecs.org.uk). Mwisho wa
maombi ni Jumatatu 29 Julai saa 5:59 usiku. 



Fanya Biashara yako ikue zaidi.

CATEGORIES

Apply For An Advert.


Email